RAIA wa Nigeria Oloasei Bogolai ambaye anakabiliwa na shitaka la kughushi hati ya kusafiria, juzi aliangua kilio mbele ya mahakama ya wilaya Ilala baada ya wadhamini aliokuwa anawategemea kutofika mahakamani.
Bongolai alifika mahakamani na kuambiwa kwamba wadhamini wake hawapo jambo ambalo lilimshitua nakuanza kulia.
Kilio hicho kilisababisha Hakimu Samwel Maweda kuingilia kati na kumwambia akimnyamazisha kwa sababu tatizo lake la dhamana bado linafuatiliwa na jamaa zake.
Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Agnes Mchome na iliahirishwa mbele ya Hakimu Maweda kutokana na hakimu husika wa kesi hiyo kutofika mahakamani.
Hakimu Maweda aaliahirisha kesi hiyo hadi Machi 4 mwaka huu.
Kupangwa kwa tarehe nyingine kwa kesi hiyo kulimfanya raia huyo wa Nigeria kuchanganyikiwa na kuendelea kushikwa na kigugumizi cha kilio huku akitetemeka.
Muda mfupi baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, alitokea jamaa yake ambaye alijitambulisha kuwa yeye ni Mwanafunzi wa chuo Kikuu Mzumbe na kwamba anafanya taratibu za kuueleza ubalozi wa Nigeria tatizo hilo ili kama kuna uwezekano ufike mahakamani kumwekea dhamana.
Baada ya kusikia kauli hiyo mshitakiwa huyo aliacha kulia na kutetemeka baada ya kuridhika na maelezo yaliyotolewa na jamaa yake huyo.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar