Jumat, 06 Februari 2009

haya sasa mastaa wetu...


Eti Jinsi Nilivyo na umbo Langu linavyovutia!!??? Ama kweli Kibaya chajitembeza! si usubiri kusifiwa na wengine?! Ila.... ni kweli! love
hayo ni maoni katika story hii

IRENE NILIWATEGA KIMPENZI KANUMBA NA RAY

ijumaa
Akiongea kwa msisitizo kwenye kipindi cha Mcheza Kwao kinachorushwa angani kupitia Runinga ya Star, Irene alisema kuwa, wakati wa uchukuaji wa filamu hiyo aliwatega kwa makusudi Kanumba na Ray kwa kuwakalia mikao ya mitego ili waweze kupata hisia za kweli wakati wanaigiza.

Irene ambaye aliwahi kuwa Mlimbwende Nambari 5 wa Tanzania mwaka 2006, alisema kuwa, filamu hiyo aliyocheza na Ray na Kanumba ilikuwa na ugumu katika kuigiza kwani kutokana na vituko alivyokuwa akiwafanyia kila dakika wasanii hao maarufu iliwalazimu kuomba ruhusa ya kwenda chooni kila mara.

“Nilikuwa najua ninachokifanya, nilikuwa nawatega ili wapate hisia za kweli za kimapenzi ili kuweza kupatikana uhalisia wa filamu na ndiyo maana kila wakati walikuwa wakiomba kwenda chooni kujiweka sawa. Ukiiangalia Oprah ni nzuri,” alisema Irene.

Akiwa anaendelea kuhojiana na Mtangazaji wa kipindi hicho, Mnyange huyo alisema kuwa, katika filamu ni lazima uweke hisia za kweli ili uweze kuleta uhalisia katika nafasi unayocheza.

“Nilicheza filamu hiyo nikijua kabisa kutokana na jinsi nilivyo, umbo langu linavyovutia ni lazima mwanaume kama Kanumba au Ray aingie mtegoni,” alisema Irene.

Filamu ya O’prah imekuwa gumzo miongoni mwa wapenda filamu za Kibongo ikidaiwa kuwa na uhalisia wa hali ya juu huku ikisemekana kuacha bifu kati ya Irene Uwoya na Wema Sepetu ambaye ni mpenzi wa Kanumba baada ya kuhisi kuna kilichokuwa kikiendelea nje ya filamu kati ya wasanii hao wawili.

Siku za hivio karibuni, imedaiwa msanii mwingine maarufu wa Bongo (jina tunalo) ameanza bifu na Irene kufuatia filamu hiyo hiyo akidai na yeye alichukuliwa ‘mali’ zake na Irene.

Habari hii inafuatiliwa kwa karibu na itakapokamilika itarushwa hewani mara moja.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar