Tuhuma dhidi ya mweka hazina wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC) ni pamoja na ugaidi, kuvunja sheria za uhamiaji na kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Chama cha MDC kimesema kukamatwa kwake ni sababu za kisiasa na kimetaka aachiliwe mara moja.
Wakati huo huo Rais Robert Mugabe na Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai, wamehudhuria mkutano wa uzinduzi wa baraza jipya la mawaziri mjini Harare.
Radio ya taifa ya Zimbabwe imetangaza Rais Mugabe aliongoza kikao hicho cha baraza la mawaziri 32.
Mwandishi wa BBC Andrew Harding akiwa mjini Johanessburg Afrika Kusini, amesema suala la mashtaka dhidi ya Bwana Bennett lilichukua nafasi kubwa ya ajenda katika kikao hicho.
Chama cha MDC kinataka Bwana Bennett aachiliwe kutoka kizuizini pamoja na wafuasi zaidi ya 30 wa chama hicho waliokamatwa katika miezi ya hivi karibuni.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar