Jumat, 06 Maret 2009

Ajali yamuua mke wa Tshangirai, yeye aponea chup chup

Mke wa Tsvangira afariki katika ajali

Waziri Mkuu wa Zimbabwe
Bw.Morgan Tsvangirai


Habari kutoka Zimbabwe zasema kua Mke wa Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki katika ajali ya barabarani.

Susan Tsvangirai alikua akisafiri na mumewe kuelekea kusini mwa mji mkuu Harare ajali hio ilipotokea.

Bw.Tsvangirai, akiwa nji kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC) aliunda serikali ya Umoja na Rais Robert Mugabe mwezi uliopita.

Msemaji wa chama cha MDC, James Maridadi, amelifahamisha shirika la habari la AP kua gari la Waziri Mkuu liligongana na Lori na Waziri Mkuu alipelekwa katika hospitali ya mjini Harare.

Ajali hiyo inatokea siku mbili baada ya Bw.Tsvangirai kulihutubia bunge kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kama Waziri Mkuuwa Zimbabwe.

Bw.Tsvangirai na marehemu mke wake Susan walifunga ndoa mnamo mwaka 1978 na hadi ajali hii walikua na watoto sita.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar