Serikali ya Sudan, imeshutumu nguvu za kimataifa zinavyotumika kuishinikiza mahakama ya uhalifu ya kimataifa (ICC), itoe hati ya kukamatwa kwa Rais Omar Hassan al-Bashir wa nchi hiyo, ikielezea mpango huo kama ukoloni mpya Afrika.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Sudan hapa nchini, Abdelbagi Kabeir, alisema baadhi ya mataifa yanayotoa shinikizo hilo si wanachama wa ICC.
Balozi huyo, aliishutumu moja kwa moja Marekani kuwa miongoni mwa mataifa yanayoshinikiza kukamatwa kwa Rais Bashir.
``Marekani si mwanachama wa ICC, lakini imekuwa mpiga propaganda mkuu wa kutaka kukamatwa kwa al-Bashir,`` alisema.
Balozi Kabeir, alisema Sudan haina uanachama katika ICC, hivyo matumizi ya mahakama hiyo yanastahili kuwepo inapohitajika na si kuchukua nafasi ya mifumo na mamlaka za kisheria za nchi hiyo.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar