Sabtu, 28 Maret 2009

Ukraine Imeathirika.je kuna mkono wa Russia?. wataalaam wanaweza kusema ni ECONOMIC COLAPSE...Serikali yatakiwa kuachia ngazi..

Waandamanaji nchini Ukraine wadai serikali ijiuzulu.

Kiev.


Waandamanaji wanaoipinga serikali nchini Ukraine wamedai kujiuzulu kwa rais Viktor Yushchenko na waziri mkuu Yulia Tymoshenko.

Zaidi ya waandamanaji 3,000 walipita katika mitaa ya mji mkuu Kiev wakiimba kauli mbiu zinazoikosoa serikali kuhusiana na jinsi inavyolishughulikia suala la mzozo wa uchumi .

Maandamano zaidi pia yamefanywa katika miji katika nchi hiyo iliyokuwa jimbo la zamani la Urusi ya zamani.

Uchumi wa Ukraine umeathirika mno kutokana na mzozo wa kifedha, lakini raia wa nchi hiyo walijizuwia kuingia mitaani hadi mwezi huu.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar