Senin, 16 November 2009

Dada Emmy ametutoka, Mungu Ametoa na Yeye ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe...



Habari zilizoifikia THE THOMCOM Inc. zinasema kuwa Dada Emiliana M. Mwidunda ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa nne (4) ambaye alitarajia kuwa daktari wa upasuaji ameaga dunia asubuhi ya leo jumatatu tarehe 16.11.2009. Familia ya Dada Emiliana M. Mwidunda na wanafunzi watanzania wanaosoma Chuo Kikuu Cha Urafiki Moscow Russia wako kwenye majonzi makubwa baada ya kuondokewa kwa mpendwa huyo. THE THOMCOM Inc. inapenda kuchukua nafasi hii kupeleka salamu za rambirambi kwa familia ya Dada Emmy, ndugu, jamaa na marafiki na kwa watanzania wote waishio moscow katika wakati huu mgumu wa kimaisha. Mungu ametoa na Mungu ametwaa. Jina la Mungu lihimidiwe






Picha mbalimbali akiwemo Dada Emmy. mojawapo ni maeneo ya kanisa moja lililoko Moscow Russia, picha iliyopigwa mara baada ya Ibada ya Misa. Picha hii ilipigwa mwaka 2006..

Tidak ada komentar:

Posting Komentar