Jua la Sahara kutoa umeme Ulaya
Mardi mkubwa wa umeme wa nguvu za jua katika jangwa la Sahara umetangazwa na makampun 12 ya biashara barani Ulaya.
Mradi huo wa kampuni ya Desertec Industrial Initiative una lenga kusambaza asilimia 15 ya umeme kwa nchi za Ulaya itakapofika mwaka 2050.
Makampuni yaliyotiliana saini mradi huo wenye thamani ya dola bilioni 400 ni pamoja na Benki ya Ujerumani (Deutsche Bank), Siemens na kampuni ya kusambaza nishati ya E.On.
Kampuni hiyo kubwa itakayokuwa na makazi yake mjini Munich, Ujerumani inatarajia kuanza kusambaza umeme barani Ulaya itakapofika mwaka 2015.
Kampuni ya Desertec Industrial Initiative ina lenga kutoa umeme wa nguvu ya jua kwa kutumia mtandao mkubwa wa vinu vya nishati na kuupeleka katika gridi za Kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar