MDC ya Zimbabwe yasitisha mgomo | ||||
Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amekitaka chama chake kusitisha mgomo dhidi ya serikali ya muungano na rais Robert Mugabe. Bw Tsvangirai amesema anampa Bw Mugabe siku 30 kutekeleza makubaliano ya kugawana madaraka, hasa kwa mambo muhimu waliojadili. Waziri mkuu huyo alizungumza hayo baada ya mkutano unaofanyika nchini Msumbiji. Bw Tsvangirai na chama chake cha Movement for Democratic Change waliigomea serikali Octoba 16. Marais wanne kutoka kusini mwa Afrika wamekutana kwenye mji mkuu wa Msumbiji, Maputo kusitisha mgomo unaotishia nchi hiyo kuzidi kuingia kwenye mgogoro. |
Sabtu, 07 November 2009
Zimbabwe tena
Langganan:
Posting Komentar (Atom)
Tidak ada komentar:
Posting Komentar