Sabtu, 07 November 2009


Zuma akizeeka atafanana kabisa na Rais Robert Mugabe kwa sura yake....comment..

Maafisa wamesema, Afrika Kusini itashindwa kutimiza ahadi ya kugawa theluthi ya ardhi kwa ajili ya kilimo kutoka kwa wakulima wazungu na kuwapa raia weusi walio wengi ifikapo mwaka 2014.

Afisa anayeshughulika na sera za urekebishaji wa ardhi, Thozi Gwanya ameiambia BBC kwamba muda huo umesogezwa mpaka 2025 kutokana na ukosefu wa fedha.

Amesema zaidi ya dola za kimarekani bilioni tisa nukta sita zinahitajika kununua ardhi iliyobaki.

Afisa wa chama cha ANC mwenye ushawishi mkubwa, Julius Malema amesema ardhi inatakiwa kunyang'anywa mikononi mwa wakulima wazungu wanaokataa kuuza ardhi zao, jambo ambalo tayari limepingwa na mawaziri wa nchi hiyo

Tidak ada komentar:

Posting Komentar