Kampuni kubwa zaidi duniani ya huduma za tafuta kwenye tovuti, Google, imejikuta matatani nchini Uswisi baada ya wenyeji kuiburuza mahakamani wakilalamikia nusanusa ya huduma ijulikanayo kama Street View.
Huduma hiyo ya kisasa imeundwa kutokana na picha zinazopigwa kwa kutumia gari yenye kamera zaidi ya sita kunasa mitaa na barabara kisha kuziunganisha na kuziweka mtandaoni kutumika kama ramani.
Hata hivyo Uswisi kupitia kamishna wake wa maswala ya faragha ya wananchi amedai kuwa picha za Street View zimekuwa zikionyesha sura za watu katika maeneo nyeti kama hospitali, magereza na shule kinyume cha sheria.
Lakini Google imedai kuwa Street View haikiuki sheria yoite na kwamba itapigana mahakamani kujitetea.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar