Minggu, 15 November 2009

Walokole wazidiwa na Mganga wa Kienyeji

Eneo la Kinyerezi, Tabata jijini Dar es Salaam, Novemba 12 mwaka huu lilikumbwa na tukio la aina yake kufuatia vita kubwa kuzuka kati ya baadhi ya watu wanaojiita walokole kutoka Kanisa la International Pentecoste Hollyness Church Ebenezer na watu wanaojihusisha na nguvu za giza ‘wachawi’ kupambana uso kwa uso mtaani mchana kweupe.

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa, walishuhudia vitu vya ajabu vikiruka angani huku nyoka waubwa na wadogo wakitoka katika nyumba ya kijana mmoja aitwaye Kafumu Moto ambaye inadaiwa ni mganga wa jadi tishio katika eneo hilo.
Walisema, tukio hilo lilianza majira ya mchana wakati kundi la walokole zaidi ya 18 likiongozwa na mhubiri maarufu katika eneo hilo aliyetajwa kwa jina moja la Kefa ambaye amepachikwa jina la Jesus, waliposambaa mtaani na kuanza kupiga injili ambayo ililenga kuangamiza uchawi, mapepo na kuleta wokovu katika eneo hilo.

Mashuhuda hao walisema kuwa, pitapita hizo za walokole, ziliishia katika nyumba ya Kafumu Moto ambapo walianza kupiga neno la mungu kisawasawa kitendo kilichomkera mganga huyo kijana na kumfanya naye kuingia ndani na kuvaa magwanda yake ya kazi ya kichawi, kisha kuchukua silaha zake za uchawi wakiwemo nyoka wakubwa na wadogo kisha kutoka nje akiwa na wapambe wake na kuanza kushambuliana na walokole hao.

Inadaiwa kuwa, Kafumu Moto aliamrisha majoka yake kuwashambulia walokole, ambao walitimua mbio na kutawanyika mtaani, huku baadhi yao wakienda kuweka kambi katika kilima kimoja porini kuendelea na maombi yao kwa sauti ya juu.

Mtandao huu ulifika eneo la tukio na kukuta mtafutano kati ya walokole na kundi la mganga huyo ukiendelea vichakani, huku watu wengine wakitimua mbio kuponya nafsi zao .

Hatimaye wahubiri watatu wakiongozwa na Kefa walikutana uso kwa uso na Kafumu ambaye alikuwa amevirigwa na nyoka mdogo shingoni huku akiwa amesheheni silaha zake ambazo ilidaiwa ni tunguli na hirizi.

Walokole walikuwa wakikemea kwa nguvu huku Mganga Kafumu naye akikemea kwa kutaja mizimu yake akiiomba iwaangamize kabisa walokole wale ambao yeye aliwaita ni wachawi wanaotumia neno la Mungu kumuangamiza.

Katika hali ya kushangaza mlokole mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Lazaro Daniel alianza kufuka moshi mkubwa ulioanzia kwenye mifuko yake ya suruali ambapo alianza kupiga kelele na kuvua suruali hiyo kisha kubakia na nguo yake ya ndani.

Baada ya Kefa kuona mwenzake akiwaka, alitimua mbio akifuatiwa na Daniel ambaye alikuwa na ‘kufuli’ aina ya Boxer huku akiomba msaada kwa watu ambao nao walianza kukimbia kuokoa nafasi zao.

Waandishi wetu walifanya jitihada za kuongea na Daniel ambaye alisitiriwa kwa kufungwa shati kwa chini, ambapo alikiri suruali yake kushika moto kimiujiza na kueleza kwamba huenda Kafumu alimwekea kiberiti.

TUKIO LENYEWE LILIKUWA HIVI.
MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Kefa (kushoto) akiwa na Daniel juu ya kilima wakipiga injili

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Mganga wa jadi Kafumu Moto akiwasili eneo la maombi kilimani.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Mganga Kafumu Moto akimwekea hirizi Daniel mfukoni.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Baada ya kuweka hirizi mfukoni kwa Daniel Mganga aliomba aombewe ili aokoke ikiwa ni hatua ya kupima uwezo wa wahubiri hao ambao walihisiwa kuwa ‘Feki’.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Ghafla Suruali ya Daniel ikaanza kuungua

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Danieli akiwa amepagawa ilibidi avue suruali yake, wakati huo mganga alikuwa akiendelea kumuombea dua ya mashetani ili azidi kukolea moto. Kushoto anayeonekana ni Mhubiri Kefa a.k.a Jesus akitimua mbio baada ya mwenzake kuanza kuwaka moto.
MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Baada ya wahubiri kutimua mbio , kilima kitakatifu cha maombi kikatekwa na kigagula Kafumu Moto.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Danieli (katikati) akiwa amejisitiri kwa kujifunga shati la mhubiri Kefa baada ya ‘kutoka nduki’. Kulia ni raia mmoja akiwa amekaa juu ya tofali mkao wa kujihami.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Kafumu Moto akiendelea kuchimba biti mtaani

MGANGA HUYO AKITOA MAELEZO BAADA YA KUMALIZIKA KWA MCHAKATO HUO (bofya hapa)


WALOKOLE WAKITOA MAELEZO YAO BAADA YA MCHAKATO HUO (bofya hapa)


PICHA:CHRISTOPHER LISSA NA ISMAIL MANG’OLA

Tidak ada komentar:

Posting Komentar