Rabu, 18 Maret 2009

Korea ya kaskazini yakataa msaada wa chakula kutoka Marekani.

Korea ya kaskazini yakataa msaada wa chakula kutoka Marekani.

Pyongyang.


Marekani imesema kuwa Korea ya kaskazini imekataa msaada zaidi wa chakula.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani na mashirika ya kutoa misaada yamesema asasi tano za Marekani zisizo za kiserikali zimeamriwa kuondoka ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, baada ya kusambaza nusu tu ya chakula walichopanga kukisambaza.

Maafisa wa mashirika ya kutoa misaada wamesema kuwa Korea ya kaskazini haikutoa sababu ya hatua hiyo.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa karibu watu milioni saba nchini Korea ya kaskazini bado wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.

Nchi hiyo imekuwa ikitegemea msaada wa chakula kutoka nje tangu njaa ya miaka ya 1990 iliyoua mamia ya maelfu ya watu nchini humo.

Kuzuiwa huko kwa misaada kunakuja wakati Korea ya kaskazini inajitayarisha kurusha satalite ambayo Marekani na washirika wake wanaiona kuwa ni kombora.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar