Sabtu, 14 Maret 2009

Madagascar yawaka moto....Africa tutaendeleaje?

Madagascar yanyemelewa na mapinduzi

Madagascar yanyemelewa na mapinduzi
Wafuasi wa upinzani wakiwa mkutanoni mjini Antananarivo
Kiongozi wa upinzani nchini Madagascar, ameonya ataongoza maandamano makubwa hadi katika kasri la Rais wa nchi hiyo, iwapo rais huyo hatang'atuka madarakani.

Kiongozi huyo wa upinzani Andry Rajoelina, aliyejitokeza kutoka mafichoni na kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Antananarivo, amempa muda rais hadi siku ya Jumamosi jioni ajiuzulu kwa "unyenyekevu".

Viongozi wa upinzani wanaojaribu kuunda serikali yao kwa sasa wanashikilia ofisi ya Waziri Mkuu.

Tangu upinzani dhidi ya serikali ulipoibuka mwezi wa Januari, watu takriban 100 wamekwishapoteza maisha yao.

Taifa hilo ambalo ni kisiwa katika bahari ya Hindi, kwa muda wa wiki saba sasa limekuwa katika machafuko yaliyosababisha uporaji, upinzani na wizi, kukiwa na mzozo wa madaraka baina ya Rais Ravalomanana na Bwana Rajoelina.

Kiongozi wa upinzani ambaye alifutwa kazi ya umeya wa jiji mwezi uliopita, alijificha tangu tarehe 5 mwezi huu wa Machi baada ya vyombo vya usalama vilipojaribu kumkamata.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar