Jumat, 27 Maret 2009

Yanga yatwaa ubingwa na mechi 5 mkononi

WAKATI kipute cha Ligi Kuu Tanzania Bara kikiwa inaelekea ukingoni huku kila timu ikiwa imebakiza mechi tano, tayari Yanga imeshatwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo, Prisons ya Mbeya imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta baada ya kuichapa Kagera Sugar 2-1.

Katika mchezo huo ambao jana ulihailishwa kutokana na mvua nyingi iliyonyesha jijini Mbeya na kusababisha uwanja wa Sokoine kujaa maji, ulishudia wenyeji Prisons ikipata bao la mapema katika dakika ya 7 lililofungwa na Yona Ndabila aliyeunganisha vema pasi ya Osward Morris.

Kagera Sugar wenye hamu ya kubwa ya kuchukua nafasi ya pili walijirekebisha katika kipindi cha pili na kupata bao la kusawazisha mwanzoni kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Shija Hassan baada ya kuchezewa vibaya kwenye eneo la hatari.
Maafande hao wa magereza waliandika bao la ushindi kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 64 iliyofungwa na Ismail Suma kwa ushindi huo sasa Prisons imefikisha pointi 25 ikiwa nyuma kwa pointi mbili kwa Simba.

Simba ina kazi ya ziada kuhakikisha inashinda mechi zake zilizosalia ili kubaki nafasi ya pili huku ikiiombea dua baya Kagera Sugar.

Mabingwa wa Tanzania Bara, ambao wamekuwa wakitumia staili yao ya 4-4-2 wameendelea kuwawashia indiketa wapinzani wao Simba ambao waliukosa ubingwa huo msimu uliopita na kushikiria nafasi ya tatu huku nafasi ya pili ambayo ilichukuliwa na Tanzania Prisons ya Mbeya.

Wakati Yanga wakishekelea kutangaza ubingwa mapema, timu za Polisi Dodoma, Villa Squad na Moro United zinapumulia kwenye mashine kutokana na timu hizo kuwa kwenye hatari ya kushuka daraja.

Katika msimamo wa ligi, Polisi Dodoma inashika mkia baada ya kucheza mechi 17 na imeshinda moja, imetoka sare mara tisa na imepoteza saba na ina pointi 12.

Villa Squad wamecheza mechi 16 wameshinda nne, wamedroo mbili na kupoteza 10 wana pointi 14 wakati Moro United ina pointi 15 ikiwa imepishana pointi moja na Polisi Morogoro, ambayo ina pointi 16.

Mechi zote zinaifanya ligi kuwa ngumu kutokana na timu zote kupambana kufa na kupona kuhakikisha zinabaki kwenye Ligi Kuu na timu za Simba, Mtibwa na Kagera wakiwania zikiwania nafasi ya kusaka Kombe la Shirikisho.

Tayari timu za Majimaji, Manyema na African Lyon zimepanda daraja na timu tatu zitashuka daraja ligi kuu.

Wafungaji waongoza kwa ufungaji msimu huu ni Boniface Ambani wa Yanga mwenye mabao (14) akifuatiewa na Hessen Bunu (JKT Ruvu) (10), Said Dilunga wa Toto Africa (8), Musa Mgosi wa Simba (7).

Tidak ada komentar:

Posting Komentar